Rais wa FIFA aliyetangaza kujiuzulu, Sepp Blatter hatahudhuria mchezo wa hatua ya fainali ya michuano ya kombe la dunia kwa wanawake utakaochezwa July 5 mjini Vancouver nchini Canada.

Babu huyo mwenye umri wa miaka 79, amechukua maamuzi hayo kwa kulinda heshima yake, kutokana na kashfa ya ulaji wa rushwa inayowaandama baadhi ya maafisa wa FIFA iliyoibuliwa hivi karibuni na shirika la upepezi la nchini Marekani, FBI.

Taarifa zinaeleza kwamba huenda Blatter akamtuma katibu mkuu wake Jorome Valke ama makamu wake wa rais, Issa Hayatou ambaye pia ni rais wa shirikisho la soka barani Afrika dunia CAF.
Sakata la ulaji rushwa linaloendelea kwenye shirikisho la soka duniani FIFA, lilipelekea Blatter kutangaza kuachia madaraka siku chache baada ya kuchaguliwa na wajumbe wa mkutano mkuu kuwa rais kwa awamu ya tano mwanzoni mwa mwezi uliopita.

Tayari timu ya taifa ya Marekani imeshakata tiketi ya kucheza mchezo wa fainali katika michuano ya kombe la dunia kwa wanawake baada ya kuibanjua timu ya taifa ya Ujerumani mabao mawili kwa moja katika mchezo wa nusu fainali.

Hii leo mchezo wa pili wa hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo itashuhudia timu ya taifa ya wanawake wa England ikipapatuana na timu ya taifa ya Japan.

Usain Bolt Awapa Ahuweni Wapinzani Wake
Kibarua Cha Nigel Pearson Chasitishwa