Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA, Joseph Sepp Blatter, amekataa kujiuzulu na badala yake amsisistiza kuendelea kukaa madarakani hadi mwezi February mwaka 2016 ambapo uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo utafanyika.

Blatter, amekataa kuachia madaraka, kufuatia tuhuma zilizoibuliwa na serikali ya nchini Usiwz kwa kumuhusisha na masuala la mlungula ambayo inadaiwa aliyafanya kwa kushirikiana na rais wa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA, Michel Platini.

Blatter ambaye tayari ameshakubali kuondoka madarakani kwa kupisha uchaguzi mkuu kufanyika mapema mwakani kufuatia sakata la baadhi ya maafisa wa FIFA kuhusishwa na masuala la mlungula tangu mwezi May mwaka huu, amesema haoni sababu ya kujiondoka kazini kwa sasa kutokana na tuhuma zilizoibuliwa na serikali ya nchini Usiwz.

Amesema ni vyema umma wa wanasoka duniani ukatambua wazi yeye hausiki na tuhuma hizo, na haoni sababu ya kuchukua maamuzi ya kujiuzulu kwa sasa ili hali ameshatangaza hadharani siku zilizopita ataondoka madarakani kupisha uchaguzi mkuu wa rais utakaofanyika mapema mwaka 2016.

Wakati huo huo rais wa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA, Michel Paltini naye ameweka msimamo wake hadharani wa kutotaka kujiuzulu kufuatia shinikizo linalotolewa na wadau wa soka kutoka pande zote za dunia.

Platini, ametangaza msimamo wake kwa njia ya barua iliyosambazwa kwenye mashirika makubwa ya habari duniani ambapo ameeleza kwa kina suala la tuhuma zilizoelekezwa kwake za kudaiwa alijihusisha na masuala ya mlungula kwa kushirikiana na rais wa FIFA Sepp Blatter.

Hata hivyo serikali ya nchini Uswiz bado inaendelea kufanya uchunguzi dhidi ya viongozi hao ili kubaini ukweli wa tuhuma zinazowakabili.

Wanasheria wa viongozi hao wawili, tayari wameshaanza kuonyesha ushirikiano na serikali ya nchini Usiwz kwa kusisitiza wateja wao hawajahusika na tuhuma nzito zinazoelekezwa kwao.

Picha: Muheza, Korongwe Wambeba Lowassa
Mourinho Aelekeza Vijembe FA