Beki wa kati wa klabu bingwa nchini Ujerumani FC Bayern Munich, Jerome Boateng amewatoa kasoro Man city kutokana na fikra walizonazio hivi sasa juu ya kiungo kiungo mshambuliaji waliyemsajili akitokea VFL Wolfsburg mwishoni mwa mwezi uliopita Kevin de Bruyne.

Boateng, ambaye aliwahi kuitumikia Man city katika msimu wa 2010-11, kabla ya kutimkia nchini kwao Ujerumani na kujiunga na FC Bayern Munich, amesema utakua upuuzi endapo wachezaji, viongozi na mashabiki wa klabu hiyo ya Etihad Stadium wakiamini De Bruyne ndio mkombozi wao.

Boateng, amesema Dde Bruyne ni mchezaji wa kawaida na anatakiwa kupewa nafasi kama walivyo wengine klabuni hapo na hakuna haja ya kutukuzwa kutokana na ada kubwa ya usajili ambayo ilitumika wakati akisajiliwa.

Amesema kuna tofauti kati ya gharama ya mchezaji pamoja na uwezo wa mchezaji, hivyo ni wakati mzuri kwa wahusika wa Man City kuendelea kukiamini kikosi chao kwa ujumla na si kumtazama mchezaji mmoja kwa kuhisi atakua na uwezo kuliko wengine.

Kevin de Bruyne alisajiliwa na Man City kwa ada ya uhamisho wa Euro million 70 ambazo ni sawa na zaidi ya paund million 50.

January Makamba: Bila Taifa Mshindi Ni Lofa
Dk Slaa Adai Anatishiwa Kupigwa Mawe, Aelekea Marekani