Msanii wa Bongo Flava, Bob Junior ambaye pia alikuwa mtayarishaji wa mziki wa Diamond Platnumz amewataka mashabiki kuliacha kama lilivyo suala lake na Diamond kwani hakuna anayejua mwanzo wa kazi zao.

Msanii huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Give Me’ amesema kuwa mashabiki wanaingilia kitu wasichokijua kiundani kitu ambacho si sawa.

“Ukweli ni kwamba hawapaswi kunizungumzia na yeye kwa sababu wakati tulikuwa tunatengenezana tulikuwa wawili, kwa hiyo huwezi kuingilia wewe kama shabiki maandazi kwa kuingilia vitu ambavyo huvijui.”

Bob Junior amesema kuwa yeye na Diamond walikuwa wanafahamiana wakati wakiwa katika chumba cha studio, baada ya hapo wakawa wakubwa, hivyo ameshangazwa na mashabikia ambao wanazungumzia kitu wasichokifahamu kuhusu wao, “sasa wewe shabiki ambaye unazungumza unamjua yeye? au unanijua mimi?, au mimi na yeye ndio tunajuana zaidi?,” amesema.

Ameongeza kuwa, “Kwa hiyo wewe unaingia kati baada ya kumfahamu Bob Junior na huyo muhusika (Diamond), unaanza kumtetea yeye au kunitukana mimi wakati sisi hatuwafamu”.

Bob Junior amekuwa akimshutumu Diamond kwa kutangaza kuwa kuna ‘kolabo’ ambayo wangefanya pamoja lakini hakuna utekelezaji na anapomtafuta ili kuzungumzia hilo amekuwa akimpuuza.

Video: Matonya ndani ya tuhuma, atajwa Diamond na Ney wa Mitego, Team Mtaa kwa Mtaa wafunguka

Trump amgeukia Rais wa Venezuela, atishia kutaifisha mali zake
Magazeti ya Tanzania leo Septemba 19, 2017