Bobi Wine amekamatwa pamoja na wafuasi wake kutokana na kukaidi agizo hilo, kwani Polisi waliweka vizuizi eneo la ufukwe Busabala ili kuhakikisha tamasha hilo halifanyiki.

Aidha, Andrewa Mukasa  na Abbey Musinguzi ambao ni waandaaji maarufu wa matamasha ya muziki, wamekamatwa pia kutokana na kuandaa tamasha hilo la Bobi Wine.

Mapema jana Aprili 21, 2019, Kamanda Msaidizi wa Polisi nchini Uganda, Assuman Mugenyi aliagiza polisi nchini humo kuzuia tamasha la mwanamuziki huyo.

Kufuatia agizo hilo, mwanamuziki aliandika kupitia mitandao ya kijamii akisema hatakubali kuacha haki zake zikivunjwa na kuonyesha atapambana hadi hatua ya mwisho ili kuhakikisha tamasha hilo linafanyika.

Meneja Man U awaomba radhi mashabiki
Video: HAUWEZI KUAMINI HILI: Kijana anayedharauliwa mtaani lakini anaingiza faida ya LAKI TATU | ASIMULIA

Comments

comments