Mshambulaji wa Simba, John Bocco amewaomba mashabiki wa mpira kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa kushuhudia timu yao ikicheza kwa mara ya kwanza mashindano ya Afrika baada ya kupita misimu mitano bila timu yao kushiriki mashindano hayo makubwa kwa ngazi ya vilabu.
Bocco amewataka mashabiki waonyeshe hamu yao ya ku-miss michuano hiyo kwa kuishangilia Simba mwanzo-mwisho lakini wao kama wachezaji watahakikisha wanapata ushindi mkubwa kwa ajili ya mashabiki na kupunguza mzigo wa mechi ya marudiano.
“Tumebeba dhamana ya mamilioni ya wapenzi wa Simba, naomba mashabiki waje kwa wingi uwanjani kuishangilia timu yao waonyeshe hamu yao ya kushiriki mashindano ya Afrika kwa kushangilia mwanzo mwisho, sisi tutapambana ili kupata ushindi mkubwa utakaoturahisishia kazi kwenye mchezo wa marudiano,”amesema Bocco
-
Young Afrcans waanza kwa ushindi kiduchu
-
Simba kuikabili Gendamarie kesho
-
Baada ya kunyimwa uwanja, Yanga kukarabati uwanja wake
Hata hivyo, leo Februari 11, 2018 Simba inatarajia kucheza mchezo wa CAF, Confederation Cup dhidi ya Gendarmerie ya Djibouti ikiwa ni mchezo wa awali katika mashindano hayo ambayo mara ya mwisho Simba kushiri ilikuwa ni Mei 2012.