Nahodha na Mshambuliaji wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC John Raphael Bocco, amesema mchezo dhidi ya Young Africans utakaochezwa Jumamosi (Mei 08), Uwanja wa Benjamin Mkapa utakuwa mgumu na wala siyo rahisi kama ambavyo watu wanafikiria.

Bocco ambaye amekosa nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza kwenye michezo kadhaa iliyopita, amesema ugumu wa mchezo huo unatokana na uzuri wa kikosi cha Young Africans ambacho kwa msimu huu kipo tofauti na ilivyokua msimu uliopita.

Amesema wanafahamu jukumu lao kama wachezjai wa Simba SC ni kuhakikisha wanasaka ushindi kwenye mchezo huo, na suala hilo ameahidi watalipambania kwa dakika 90, lakini amewataka mashabiki na wanachama kuwa watulivu na kuamini mchezo utakua mgumu.

“Mchezo utakuwa mgumu na wala siyo rahisi kama ambavyo watu wanafikiria, Yanga wanacheza vizuri tangu mwanzo wa msimu, lakini sisi tuna wachezaji bora na tutajipanga na kuondoka na alama tatu.

“Niwaombe mashabiki waendelee kutusapoti kwa kuwa tupo tayari kwa ajili ya mchezo huo na tutapambana ili kufanya vizuri,”  amesema Bocco.

Simba SC inakwenda kucheza mchezo wa Jumamosi (Mei 08) ikiwa inaongoza msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kufiksha alama 61, ikifuatiwa na Young Africans yenye alama 57 huku Azam FC wakishika nafasi ya tatu kwa kufikisha alama 54.

Kocha Gomes asuka mipango kabambe
ATCL yasitisha safari za India