Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes amewaandalia programu maalumu washambuliaji wake Chris Mugalu, John Bocco kwa ajili ya kuwaongezea makali ili waweze kucheka na nyavu.

Simba inatarajiwa kuvaana na AS Vita kesho Jumamosi (April 03) katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa saa kumi kamili kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Washambuliaji hao walipewa program maalum ya jinsi ya kufunga mabao pekee muda mfupi baada ya kumalizika kwa mazoezi ya jumla ya kikosi cha timu hiyo.

Katika mazoezi hayo yaliyofanyika Simba Mo Arena, Bunju, Dar es salaam, kocha huyo alimtaka kila mshambuliaji apige shuti au kumchambua huku akiwatengea kila mmoja mipira kumi kwa ajili ya kupiga golini na kufunga.

Gomes aliwatengea mipira hiyo nje ya 18 na kuwataka kupiga golini kwa ajili ya kufunga na lengo likiwa ni kuwaongezea umakini wanapofika katika eneo la hatari la wapinzani wakiwa katika maandalizi ya mchezo dhidi ya AS Vita.

Kocha huyo alitumia program hiyo kwa zaidi ya dakika 15 kwa kila mmoja kupiga mashuti 10 kwa kubadilishana huku golikipa akiwa Beno Kakolanya.Program hiyo iliwataka mastaa hao kupiga mashuti kwa kubadilisha miguu, kulia na kushoto, kabla ya baadaye kuwaongezea program ya kupiga mipira kwa kichwa.

Mipira hiyo ya vichwa ilikuwa inapigwa kutokea pembeni na kiungo mshambuliaji raia wa Kenya, Francis Kahata ambayo kati ya hiyo Bocco alifunga bao moja, huku mingine tisa ikiishia mikononi mwa Kakolanya.

Kwa upande wa Mugalu, hakufanikiwa kufunga.Akizungumzia kuhusu safu yake ya ushambuliaji, Gomes amesema: “Safu yangu ya ulinzi imekuwa ikifanya vizuri sana lakini safu yangu ya ushambuliaji imekuwa inashindwa kutumia kwa ufasaha nafasi tunazotengeneza, jambo ambalo ni lazima tulifanyie kazi.

NCCR Mageuzi yaungana na CHADEMA, yasusia uchaguzi
Rashford amtaja Sadio Mane EPL