Waziri wa Fedha na Mpango Dkt. Mwigulu Nchemba amependekeza kupunguza tozo kwa makosa ya madereva bodaboda na Bajaji kwa makosa yanayofanywa barabarani ambapo amesema itakuwa Sh. 10,000 badala ya sh. 30,000 kwa kosa moja.

Amesema hayo wakati akiwasilisha Bajeti kuu ya Serikali mwaka 2021/22 Bungeni Jijini Dodoma leo Juni 10, 2021 ambapo amesema lengo la faini hii ni kuweka adhabu kwa kuzingatia uwezo wa kulipa.

Amesema vijana wengi wamejiajiri kwenye biashara ndogondogo ambazo zinajulikana kama bodaboda.

Hali hii imekuwa ikisababisha wengi kushindwa kulipa faini na hivyo kuzitelekeza pikipiki zao kwenye vituo vya polisi.

”Rais Samia Suluhu Hassan alilielekeza Jeshi la Polisi kujikita kwenye kutoa Elimu badala ya kuwekeza kwenye makosa na kugeuza faini kuwa chanzo cha mapato” amesema Nchemba

Waziri nchemba amesema kuwa vijana hawa wanapata usumbufu mkubwa wa kulipa faini kutoka kwenye vipato vyao pale panapotokea uvunjaji wa sheria ya usalama barabarani.

Tanzania na Botswana kuendelea kushirikiana
Mayay ajitosa Urais TFF