Bodi ya watendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Imeandaa mkutano mkubwa wa kuwakutanisha na wasanii wote nchini kesho Juni 28 katika ukumbi uliyopo ofisi za BASATA jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti wa BASATA, Habbi Gunze amesema kuwa mkutano huo na wasanii nchini utakuwa wakwanza tangu bodi mpya ya watendaji ilipoteuliwa mwishoni mwa mwaka jana.

Na ameeleza lengo kuu la kukutana na wasanii ni kufahamu changamoto zinazowakabili ili wasifanye maamuzi kwa nadharia, na kujadili mipango mikakati ya kuendeleza sekta ya sanaa hapa nchini Tanzania.

” kwakuwa kazi ya bodi hii ni kufuatilia kazi za BASATA na kufanya maamuzi ni jambo zuri ikakutana na wasanii wenyeywe ili tujadiliane na kupanga mipango mikakati ya muda mfupi na ile ya muda mrefu” amesema Gunze.

Halikadhalika ametoa wito kwa wasanii wote wa sanaa za muziki, filamu na sanaa za ufundi kuhudhuria kwani michango yao wanaithamini sana na ndiyo itakayoleta maendeleo kwenye sanaa.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Juni 28, 2019
Taifa Stars uso kwa uso na Harambee Stars