Ni baada ya sakata la kuwasaka wanafunzi hewa  waliohifadhiwa na bodi ya mikopo,   bodi ya mikopo yaanza rasmi kuingiza fedha za mkopo  awamu ya pili kwa ajili ya  mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.

Kutokana na taarifa hiyo bodi ya mikopo ilitoa ufafanuzi kuhusiana na wanafunzi ambao hawajakamilisha  uhakiki wa taarifa zao za mkopo kuwa zoezi la uchambuzi wa barua zilizoandikwa na wanafunzi ambao hawakufanya uhakiki kwa mara ya kwanza linaendelea,  ili kupitia sababu zilizofanya wanafunzi  hao wasihakiki  ili waweze kuhakikiwa  upya.

Pia bodi ilitoa msisitizo kwa wanafunzi ambao bado hawajandika barua ya kutoa sababu zilizofanya wasifanye uhakiki  kuandika barua  hizo na kuomba kuhakikiwa upya.

Video: Hotuba ya Trump yakatishwa Kanisani, Mchungaji amgeuka
Mwanafunzi Kidato cha Kwanza ajifungua bwenini