Wakuu wa mashirika mawili makubwa ya kutengeneza ndege duniani Boeing na Airbus Amerika Kusini wametoa wito kwa serikali ya Marekani kusitisha kusambaza huduma mpya za simu za 5G.
Aidha watendaji wa makampuni hayo Dave Calhoun na Jeffrey Knittel, katika barua waliyoiandika kwa Waziri wa Usafiri wa Marekani Pete Buttigieg wameionya teknolojia hiyo inaweza kuwa na athari mbaya kwa sekta ya usafiri wa anga kama mita za urefu wa redio.
Barua hiyo ilinukuu utafiti wa shirika la biashara la Airlines for America ambao uligundua kuwa ikiwa sheria za Shirika la Usafiri wa Anga (FAA) 5G zingetumika mnamo 2019, takriban ndege 345,000 za abiria na safari 5,400 za mizigo zingekabiliwa na ucheleweshaji, ubadilishaji au kughairiwa.
Mashirika kadhaa ya ndege yamesema kuwa hatua hizo hazikidhi mahitaji, baada ya Boeing na Airbus kusema walitoa pendekezo mbadala ambalo lingezuia usambazaji wa simu za rununu karibu na viwanja vya ndege na maeneo mengine muhimu
Wiki iliyopita, afisa mkuu mtendaji wa shirika la ndege la United Scott Kirby alisema maagizo ya FAA ya 5G yatazuia matumizi ya simu hizo katika takriban viwanja 40 vikubwa zaidi vya ndege nchini Marekani.
Mashirika ya teknolojia ya Marekani yanasema 5G ni salama na kulaumu mashirika ya ndege kwa kutoa taaarifa za kuogogya na za kupotosha kuhusu teknolojia hiyo.