Kundi la kigaidi la Boko Haram lenye makazi yake nchini Nigeria, limewaua waumini 150 wa dini ya kiislam waliokuwa wakiswali katika msikiti nchini humo.

Mashuhuda wameeleza kuwa wanamgambo zaidi ya 50 wa kundi hilo wakiwa na bunduki walivamia vijiji vilivyopo kaskazini mashariki mwa Borno na kuwaua kwa wanawake waliokuwa wakitayarisha chakula huku wakiwachomea ndani ya nyumba baadhi ya wakazi wa vijiji hivyo.
corps
Hili linatajwa kuwa tukio baya zaidi kufanywa na kundi hilo katika kipindi cha wiki tano huku majeshi ya Nigeria yakiwaandama wanamgambo hao na kusambaratisha baadhi ya ngome zao.

Rais Muhammadu Buhari ameahidi kuwa kupaumbele chake ni kupambana na kundi hilo na tangu alipoingia madarakani wiki tano zilizopita majeshi ya Nigeria yakisaidiana na nchi jirani yameziandama ngome za wanamgambo wa jeshi hilo.

Boko Haram ambao wanawashikilia wasichana zaidi ya 200 na kuwatesa huku wakiwapa mafunzo kuwa magaidi limekuwa likifanya matukio makubwa ya mauaji nchini humo kwa kushtukiza na kuvizia.

Muhanga Wa Tsunami Asajiliwa Sporting Lisbon
Mama Wa Chris Brown Amponza Mkwewe