Bingwa mara sita wa medali za dhahabu kupitia michuano ya riadha inayotambulika duniani Usain Bolt, ametoa msaada ya vifaa vya michezo vyenye thamani ya dola za kimarekani million 1.3 sawa na paund million 838, katika shule aliyosoma nchini Jamaica.

Bolt anayetamba katika mbio za mita 100 na 200, alidhihirisha hilo kwa vitendo baada ya kufika kwenye shule ya William Knibb Memorial High School, na kuwasilisha msaada wa vifaa vya michezo ambavyo anaamini vitasaidia kuendeleza michezo shuleni hapo pamoja na taifa la Jamaica ili kuwapata watetezi wengine katika nyanja hiyo duniani kwa miaka ijayo.

Vifaa vya michezo vilivyotolewa na mwanariadha huyo ni mipira 50 ya soka, vilinda ugoko (Shin Guards), jezi za mazoezi (Bibs) ambavyo vyote kwa pamoja na vina nembo ya Usain Bolt ambayo inaalama ya mtu aliyenyoosha mikono upande mmoja.

Man Utd Waanguka Tena Kimapato
Luke Shaw Kupigwa Kisu Tena