Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani amesema mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi utapita katika mikoa minane (8) na vijiji 184 hapa nchini.

Amesema vijiji hivyo vinapatikana katika wilaya 24 zilizopo katika mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara na Tanga. Bomba hilo litagharimu shilingi trilioni 8, likiwa na urefu wa kilomita 1,450.

”Katika vijiji hivyo watapitiwa na fursa za mradi, ajira 10,000, wakati wa ujenzi zitapatikana na itasaidia kupunguza umaskini, pia kuna megawati 35 zitapatikana kupitia mradi huo” amesema Medard.

Hayo amezungumza leo Jumamosi wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka HoimaUganda mpaka Chongoleani Tanga.

Rais Yoweri Museven na mwenyeji wake Rais John Pombe Magufuli pamoja na Serikali wameongoza sherehe hizi wakiwa wameambatana na mawaziri, wabunge huku wananchi wakiwa wamejitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hilo la kihistoria likitokea nchini Tanzanai.

Korea Kusini yakubali yaishe, yataka mazungumzo yafanyike
Uhamiaji yafanya mapinduzi yaja na mfumo mpya maombi ya pasipoti