Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar-es-salaam (DAWASA), imetoa taarifa kwa Wananchi na Wakazi wa Bagamoyo hadi Kigamboni kuwa huduma ya majisafi itakosekana kwa saa 24 kuanzia leo Juni 8, 2021 asubuhi hadi kesho June 09,2021 kufuatia dharura ya kupungua kwa uzalishaji maji mtambo wa Ruvu Chini.

DAWASA imeeleza sababu za kukosekana maji kwa muda huo kuwa ni kupisha matengenezo ya bomba kuu la usambazaji maji lenye inch 54 linalotokea katika matenki ya Chuo Kikuu Ardhi eneo la Victoria na Makumbusho baada ya bomba hilo kupasuka.

Maeneo yatakayoathirika ni Mji wa Bagamoyo, vijiji vya zinga, Kerege, Mapinga, Bunju, Boko, Mivumoni, Kawe, Kinondoni, Ilala, Temeke, Uwanja wa Ndege, Tegeta, kunduchi, Salasala, Jangwani, Mbezi Beach, Mlalakuwa, Mwenge, Mikocheni, Msasani, Sinza, Kijitonyama, Oysterbay na Magomeni.

Maeneo mengine yatakayoathirika ni Upanga, Kariakoo, katikati ya jiji (City center), Ubungo Maziwa, Kigogo, Mburahati, Hospitali ya Rufaa Mhimbili, Kigamboni Navy na Ferry.

Serikali kuanzisha vituo vya kulea vipaji
Mzindakaya afariki dunia, kumbe aliwahi kuvuliwa Ubunge na Mahakama