Hili ni bomba la bafuni lenye uwezo wa kubadilisha rangi kuonesha kama maji ni ya moto ,baridi au vuguvugu.

Shukrani za dhati zinaifikia teknolojia ya kisasa ,kwa uvumbuzi wa wa vitu mihimu na rahisi kama njia imara na bora wakati wa  kuoga.

Kutokana na watu kuwa na msongamano wa majukumu usalama umekuwa ukipungua kwa kiasi fulani lakini teknolojia ya kisasa inalipa bomba la bafuni uwezo wa kuonesha mabadiliko katika hali ya joto la maji yanayotiririka kupitia bomba hili bafuni kwako.

.Katika  nyumba zenye mfumo wa kawaida wa maji moto , unajua jinsi unavyoweza kukasirika kwenda bafuni kuoga asubuhi yenye baridi kali na matarajio kuwa unaoga maji ya moto lakini tu ukikuta yanatoka maji ya baridi inakuwa sio kitu kizuri.

Bomba hufanya kazi kwa muundo rahisi,lakini mwanga angavu ambao hubadilisha rangi za taa ya LED iliyowekwa kwenye bomba mara moja hugundua na kuonesha mabadiliko katika hali ya joto ya maji yanayotiririka ndani yake.

Wakati ni maji baridi (30-32 °C),hutoa taa ya samawati; maji ya joto (31 – 40 °C) hutoa taa ya kijani kibichi ; maji ya moto (41- 50 °C ) hutoa taa Nyekundu; na maji ya moto sana (51 – 100°C ) itafanya LED itoe taa nyepesi kama  onyo ili kuzuia taa nyekundu kuwaka. 

Bomba hili linauzwa kiasi cha  dola za kimarekani 74.99.

Jaji wa Mahakama ya Juu Marekani afariki
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Septemba 19, 2020

Comments

comments