Operesheni ya Bomobomoa iliyowakabili watu wanaoishi katika maeneo ya wazi na mabondeni tangu ilipoanza, sasa imeanza kuwafyeka watu waliojenga katika fukwe za bahari.

Zoezi hilo la Bomobomoa leo limeiukumba ufukwe maarufu wa Coco Beach jijini Dar es Salaam ambapo serikali imevunja uzio wa ufukwe huo uliojengwa kinyume cha sheria.

Naye Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo  ya Makazi, William Lukuvi ameagiza watendaji wote wa serikali waliodaiwa kutumia ofisi zao kutoa vibali vya ujenzi kinyume cha sheria wasimamishwe na kufanyiwa uchunguzi.

Waziri Lukuvi alisema kuwa ripoti ya ukaguzi wa watumishi hao wa serikali ambao wamebainika kuwa walishiriki kutoa vibali kinyume cha taratibu iwasilishwe kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

 

 

 

Tundu Lissu: Wanaamini Bunge Limekuwa Hatari... Tutapambana
Majangili watungua helikopta ya Doria Kusini mwa Mbuga za Serengeti