Wanafunzi sita wa shule ya msingi Kihinga mkoani Kagera wamefariki dunia na wengine zaidi ya 40 wamejeruhiwa baada ya kutokea kwa mlipuko unaosadikiwa kuwa ni bomu kutokea shuleni hapo.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Kagera, Augustine Orom huo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na tayari wananchi wamejitokeza kuchangia damu kwa ajili ya kuwasaidia majeruhi.

Kwa mujibu wa Daktari Mariagoreth Fredrick ambaye ni mganga mkuu hosipitali ya Rurenge, amethibitisha kupokea miili hiyo na majeruhi ambao baadhi wako katika hali mbaya na tayari wanapatiwa matibabu.

“Tulionao hali ya sio nzuri. Wengine wameumia matumbo, wengine wamechanika bandama, wengine wamevunjika miguu, wengine vichwa vimepata majeraha, wengine wameumia macho,” amesema Daktari

Inaelezwa kwamba kabla ya kulipukiwa na kifaa hicho kinachoarifiwa kuwa ni bomu, wanafunzi hao walikuwa wanakikichezea.

Idadi ya waliofariki kwa mlipuko Kagera yaongezeka
Majaliwa apiga marufuku Mawaziri kutoa matamko