Bondia Tony Rashid ambaye mwezi uliopita alifanikiwa kushinda ubingwa wa Afrika Mashariki na kati dhidi ya Haidari Mchanjo katika pambano ambalo lilifanyika club 361, Mwenge jana ameshinda ubingwa wa ABU.

Pambano hilo lililofanyika nchini Afrika Kusini lilikuwa na ushindani ambapo Tony alishinda kwa TKO raundi ya 11 akimshinda mpinzani wake wa Afrika Kusini.

Rashid amesema kuwa maandalizi mazuri yalimbebba kwenye pambano hilo na kumpa nafasi ya kuibuka na ubingwa huo.

“Nilijipanga na kufanya mazoezi ya kutosha kwa ajili ya pambano, shukrani kwa mashabiki kwa sapoti pamoja na jamaa wote ambao nipo nao.

“Natarajia kurejea leo majira ya saa 11:00 jioni ningependa mashabiki wajitokeze kuupokea ubingwa wao ambao nimeupata,” alisema Mchanjo.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Septemba 17, 2019
Rais Magufuli apiga marufuku tozo machinjio ya Vingunguti