Bondia wa kike,bingwa wa dunia ambaye hajawahi kupoteza shindano hata moja, Ronda Rousey ameendelea kumchokoza Floyd Mayweather tangu atambe kuwa ana uwezo wa kumpiga.

Ronda Rousey ameendeleza vita ya maneno dhidi yake na Floyd hasa baada ya Floyd kudai kuwa mwanamke huyo hana hadhi ya kuwasiliana naye kwa kuwa hana fedha kama yeye akimtaka amtafute baada ya kuwa na uwezo wa kutengeneza $300 million kwa usiku mmoja.

“Niliona Mayweather alivyosema, ‘ukiweza kutengeneza $300 million kwa usiku mmoja unaweza kunipigia.’ Na niliamua kufanya mahesabu. Kwa kuzingatia kiasi nilichotengeneza kwenye pambano langu la mwisho, mimi ni bondia wa UFC ninaelipwa zaidi na ni mwaname,” alismea Rousey.

“Na ninadhani nataengeneza pesa mara 2 hadi 3 zaidi ya anazoingiza kwa sekunde. Kwa hiyo siku atakapojua kusoma na kuandika anaweza kuni-text,” mwanamke huyo alimkejeli Mayweather.

Baada ya kuona ujumbe huo, mayweather ambaye hawezi kunyamaza alimtumia mtu wake wa karibu kuiambia TMZ akimkumbusha kuwa yeye ndiye aliyetajwa na Forbes kuwa anaongoza kwenye orodha ya wanamichezo wanaoingiza fedha nyingi.

“Mara ya mwisho niliangalia Forbes nilikuwa nafasi ya kwanza. Hauweza kuwa na hadhi yangu. Endelea kutafuta umaarufu.”

Mbali na ndondi, Ronda pia anasifika zaidi kwa kucheza Martial Art na Judo.

 

Stars Kupambana Na Libya Kesho
Miss Tanzania Yatangaza Kamati Mpya, Jokate Apewa Shavu