Siku zote waswahili wamekua na usemi usemao “Unapofanya Jambo La Kheri, Usitegemee Kulipwa Kheri”  na mara nyingi hali hii huwakuta wenye moyo safi wa kuwasaidia wengine, lakini hukosa fadhila kutoka kwa wanaowasaidia.

Katika mchezo wa soka makocha wengi hujitoa kwa ajili ya kuwasaidia wachezaji vijana wenye vipaji, lakini hukosa msaada kutokana na mazingira wanayoishi.

Ndivyo ilivyokua kwa mchezaji Bongani Zungu kijana wa Afrika kusini mwenye umri wa miaka 27, ambaye alipewa msaada wa kisoka na kocha Pitso ‘Jingles’ Mosimane.

Zungu alikua mchezaji wa kawaida tu kutoka Pretoria University, ila jicho la Mosimane linaona tusivyoona, linasoma visivyoandikwa alikigundua kipaji hiki, alitumia muda wake kumshawishi Tycoon Patrick Motsepe amchukue.

Mosimane alifunga safari mpaka Duduza, nyumbani kwa Zungu ili kumwambia nakuhitaji Mamelodi Sundowns, nakuhitaji pale Masandawana bila shaka ni ndoto ya watoto wengi kwa Mandela kucheza pale, Buhle Mkhwanazi alitolewa kama chambo.

Zungu alikua winga ya kulia, ila Mosimane alimwambia huna kasi ya kucheza pembeni wewe sio Cristiano Ronaldo, ni mzito huna kasi kijana, nitakupeleka kati ila sio namba 10 kwakua huna jicho la goli wewe sio Messi, nitakusimamisha namba nane, una akili kama Steven Pienaar.

Bila shaka unaikumbuka Mamelodi ile, wana watu hatari kikosini kwao una Keagan Dolly, Percy Tau, Thabho Nthethe, Khama Billiat, Hlompho Kekana na Dennis Onyango, lakini ndani humo Zungu alicheza kwa kiwango kutokana na mapenzi ya Kocha.

Bila shaka tunakumbuka safari ya Zungu kuelekea Vitoria Guimares ya Ureno, 2016 ndipo huko alianza kumvunjia heshma Kocha wake, baada ya kutwaa ubingwa ule wa Afrika kijana alitweet kuwa kazi kubwa alifanya Msaidizi Rhulan Mokoena na sio Mosimane.

EXTRA TIME: Watch Mosimane doesn't believe Bongani Zungu wrote ...
Pitso ‘Jingles’ Mosimane

Mosimane alimchukulia Zungu kama mtoto wake aliemlea, aliweka wazi kuwa Mtoto wake kamnyea nae hatokata kiganja, alichangua kuthamini zaidi kipaji cha mtoto aliemlea na kumkuza.

Zungu ni moja kati ya mafundi pale Bafana Bafana, tunakumbuka pacha yake na Dean Furman ilisimbua sana AFCON 2019, huyu ni Kiungo tegemeo pale Amiens ya Ufaransa, akicheza kwa madaha na ubishoo mkubwa sana. Zungu anatokea mitaa ya Duduza pale Gauteng, mji ambao wanaishi watu wa maisha ya chini, ndipo ilipo maskani ya fundi wa Mpira karibu tu na Soweto.

Lusajo asitisha mpango wa mkataba mpya Namungo FC
Simba SC yaendelea kutesa Afrika