Baada ya kudorora kwa soko la filamu hapa Bongo na Afrika Mashariki kwa ujumla, licha ya tasnia hiyo kuajiri vijana wengi lakini imezidi kupoteza mvuto kwa mashabiki wake mara baada ya kukosekana kwa ubunifu.

Kupitia kampuni ya Candy and Candy ya nchini Kenya ambayo imefungua tawi lake hapa jijini Dar es salaam imeamua kuandaa kongamano maalum ambalo litawakutanisha wadau mbalimbali wa filamu kutoka mataifa ya Afrika Mashariki na Kati lijulikanalo kama ‘TAKEU Film Expo’ kwaajili ya kujadili changamoto zinazowakabili.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Joe Kariuki alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, amesema kuwa Kongamano hilo litakuwa mahususi kwaajili ya kuangalia namna ya kukabiliana na changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili katika tasnia hiyo ambayjo kwa sasa imeonekana kukosa mvuto kwa siku za hivi karibuni.

“Nia yetu ni kuipeleka tasnia ya filamu hapa Bongo na East Africa kwa ujumla kimataifa zaidi ambapo ukitazama hapo awali Bongo movie ilikua juu sana lakini kwasasa inaelekea kupoteza mashabiki,so nipo kwa ajili ya kurudisha hadhi hiyo,”amesema Kariuki

 

Superior Paper Topics
Video: Aliyosema Tundu Lissu kuhusu uamuzi wa Rais Magufuli