Mgombea ubunge wa jimbo la Kongwa mkoani Dodoma na aliyekuwa spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amewaomba wananchi wa Urambo, kumchagua na kumpa ushindi wa kishindo Dkt. John Magufuli, pamoja na mgombea ubunge Magreth Sitta, ambapo watapata nyongeza ya mbunge wa viti maalumu.

Ndugai, ametoa kauli hiyo leo Septemba 21, 2020, katika mkutano wa kampeni za CCM, wakati akimuombea kura mgombea urais kupitia CCM Dkt. John Magufuli, pamoja na mgombea ubunge wa jimbo la Urambo kupitia chama hicho, Margareth Sitta.

“Sisi wa CCM tunaomba kura tatu ya kwanza ya Rais, wabunge na madiwani na hapa Urambo namuombea Mama Margareth Sitta na ukipiga kura kwa Magufuli na Mama Sitta kwa Urambo hapa unapata ‘bonus’ kwa sababu mtampata mbunge wa Viti Maalum anaitwa Jackline,” amesema Ndugai

”Tusichague wapinzani kwa sababu tatizo lao ni kupinga kila kitu, Rais Magufuli akitaka kujenga reli wanapinga, akitaka kujenga barabara na kusambaza umeme na akitaka kutoa maji Ziwa Victoria kuleta Urambo wanapinga sasa mtu wa namna hiyo wa nini,” ameongeza Ndugai.

Kinachoisumbua Namungo FC chaanikwa hadharani
Mbaroni kwa madai ya kumuozesha mwanafunzi

Comments

comments