Kampuni ya Boomplay na Universal Music Group zimeingia mkataba wa usambazaji wa muziki katika masoko mengi ndani ya Afrika.
UMG ni kampuni ya kwanza ya muziki kupitisha leseni yake kwa Boomplay, ambayo inajulikana kwa huduma yake ya kusikiliza muziki barani Afrika.
Chini ya makubaliano ya mkataba huo wa miaka mingi na ufanisi, Boomplay itasambaza muziki kutoka kwa UMG nchini Tanzania pamoja na nchi za Nigeria, Ghana, Kenya, Rwanda, Uganda na Zambia.
Aidha, watumiaji wa Boomplay sasa wanaweza kupata nyimbo za nyumbani na za kimataifa kutoka UMG wakiwemo wasanii kama Eminem, Tekno, Post Malone, Nicki Minaj, Lady Zamar, Lil Wayne, na wengine wengi.
Mapema mwaka huu, UMG ilitangaza uzinduzi wa Universal Music Nigeria, ikiwa na lengo la kuwapa wasanii fursa nyingi barani Afrika kwaajili ya kufanikisha kazi zao kufika hatua za kimataifa, ikiwa na lengo la kukuza mazingira ya muziki wa Afrika pamoja na kurekodi muziki, kuchapisha muziki, uzalishaji, matamasha, ushirikiano wa makampuni na jitihada za biashara.
-
Jermaine Dupri atoa mtazamo tofauti kwenye fainal za Super Bowl
-
Usher aiomba mahakama usiri wa gonjwa la ngono
-
Michael Jackson aibuka kinara marehemu wanaoingiza pesa ndefu
Kwa upande wake makamu wa Rais wa Universal Music Group, idara ya Maendeleo ya Masoko, Adam Granite amesema kuwa wanatarajia kufanya kazi na Boomplay ambapo watawawezesha wasanii wa Kiafrika kuwa wabunifu, kuendeleza masoko na uendelezaji wa rasilimali ili kuharakisha kazi zao zinaendelea kukua barani Afrika.