Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad amesema kuwa hana ndoto za kuhamia CCM kwakuwa haridhishwi na utendaji kazi wa chama hicho.
Ameyasema hayo Kilimahewa Visiwani Zanzibar wakati akizindua Jumuiya ya Wazee wa chama hicho (JUZECUF), ambapo amesema kuwa wakati wa ukoloni hakukuwepo kukamatwa kwa watu kama sasa inavyofanyika.
Amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinatakiwa kuelewa kuwa Tanzania ni ya Watanzania hivyo hawawezi kutawala wanavyotaka.
“Leo hii kila sehemu unasikia diwani ama mbunge kaingia CCM tena kwa tamko maalumu, mliona wapi, Mwenyekiti wa Kijiji akishakuwa CCM tu basi anaweza kuamrisha jeshi la polisi likukamate na unakamatwa kweli na kuwekwa ndani,”amesema Maalim Seif
Hata hivyo, kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Amour Said Mohamed amesema kuwa kwa kushirikiana na wazee wenzake watahakikisha chama kinasonga mbele na kutoa ushauri wakati wowote unapohitajika.
-
Dkt. Bashiru aikana kauli yake, adai Bashe, Nape sio watukutu
-
Mrema awatangazia kiama wanao mtolea lugha chafu JPM
-
Prof. Lipumba aitaka CCM kuacha kupandikiza usaliti ndani ya CUF