Klabu ya Borussia Dortmund huenda ikafanikiwa kumrejesha kiungo Mario Gotze, baada ya kuonekana hatoweza kuendana na mipango ya meneja mpya wa FC Bayern Munich, Carlo Anceloti.

BVB wamejizatiti kumrejesha nyumbani kiungo huyo mwenye umri wa 24 kwa kuamini bado ana nafasi ya kudhihirisha ubora wake, japo ameonekana ameishiwa cheche za kufanya vyema chini ya utawala mpya ambao utaanza kazi mwezi ujao huko Allianz Arena.

Taarifa zilizochapishwa kwenye gazeti la Daily Mirror la nchini England, zinaeleza kwamba viongozi wa Borussia Dortmund wameonyesha dhamira ya kweli katika usajili wa Gotze, kutokana na ushindani uliopo dhidi ya Tottenham Hotspurs ambao wapo tayari kumuhamishia kaskazini mwa jijini London.

Tayari mazungumzo ya awali kati ya viongozi wa FC Bayern Munich dhidi ya Spurs na BVB yameshafanyika na kinachosubiriwa kwa sasa ni mustakabali wa muhusika kuona ni wapi patakapomfaa kucheza soka lake baada ya kuondoka mjini Munich.

Hata hivyo inaelezwa kwamba, kuna uwezekano mkubwa kwa Gotze kuchagua kubaki nchini Ujerumani, kutokana na kuyatambua vyema mazingira ya soka la nchini humo, tofauti na itakavyokua pindi atakapofanya maamuzi ya kuelekea nje ya nyumbani kwao.

Gotze, aliondoka Dortmund na kujiunga na FC Bayern Munich mwaka 2013, na kwa sasa ameweka sokoni kwa thamani ya Pauni milion 20.

Audio: Hatuna Hofu na Mkutano Wowote wa CCM - Mbowe
Everton Waitoa Jacho Chelsea Kwa Kalidou Koulibaly