Mmoja wa wajumbe wa Klabu ya Real Madrid ametoa siri kuwa Mshambuliaji wa Paris St-Germain na Ufaransa, Kylian Mbappe anataka kujiunga na timu yao katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi wakati mkataba wake wa sasa utakapomalizika.

Mbappe mwenye umri wa miaka 24, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwakani na amegoma kusaini dili jipya.

Mbappe ambaye msimu huu amecheza mechi tisa za michuano yote na kufunga mabao manane, anahitajika pia na baadhi ya timu barani Ulaya.

Staa huyu wa kimataifa wa Ufaransa aliingia kwenye mgogoro na mabosi wa PSG baada ya kugoma kusaini kipengele cha kuurefusha mkataba wake kufikia mwaka 2025.

Mbali ya Madrid, saini ya Mbappe pia imekuwa ikiwindwa na baadhi ya vigogo nchini Saudi Arabia lakini yeye mwenyewe mpango wake zaidi kutua nchini Hispania.

Hadi sasa viongozi wa PSG wameendelea kushikilia msimamo wa kutotaka kumuachia Mbappe na bado wana matumaini ya kwamba atasaini mkataba wa kuendelea kusalia kwenye timu yao kabla ya msimu huu kumalizika.

Watanzania wanataka umeme - Dkt. Biteko
Viongozi wakielewe Kilimo ili kuwaelimisha Wakulima - Malima