Makamu wa Rais wa Sevilla, lose Maria Carrasco amefichua mpango wa Sergio Ramos iwapo atafunga dhidi ya klabu yake ya zamani ya Real Madrid baadae leo Jumamosi (Oktoba 21).
Mshindi huyo wa Kombe la Dunia mwaka 2010 alirejea katika kikosi cha Sevilla kama mchezaji huru baada ya mkataba wake na Paris Saint Germain kipindi cha usajili wa kiangazi.
Baada ya kukaa kwa muda wa miaka 10 katika jiji la Madrid ambapo aliiongoza Madrid kutwaa mataji mengi ya ndani na Ulaya, leo atakabiliana na wachezaji wenzake wa zamani kwa mara ya kwanza akiwa amevalia jezi ya Sevilla.
Hata hivyo, Carrasco anaamini beki huyo atajizuia kusherehekea iwapo atafunga bao.
“Nadhani hatasherehekea. Sijamuuliza, lakini nadhani hatasherehekea. Ingawa anatoka Seville na alikulia hapa, Ramos ana nyumba mbili Sevilla na Real Madrid” aliiambia Radio MARCA.
Ramos amepokelewa vizuri tangu alipotua Sevilla na alijumuishwa katika kikosi kilichocheza dhidi ya Barcelona kwenye mechi ya La Liga.
Ingawa Ramos atakuwa na hamu ya kuonyesha uwezo wake dhidi ya Madrid, kutokana na mazingira magumu yaliyochangia kuondoka na itashangaza iwapo atasherehekea bao endapo atafunga kwa mara ya kwanza dhidi ya timu yake ya zamani.