Uongozi wa Simba SC, umesema timu yao itaushangaza ulimwengu kwa kuifunga Al Ahly kwenye mchezo wa Robo Fainali ya African Football League.

Hayo yamejiri baada ya Simba SC kupangwa kucheza na Al Ahly, Oktoba 20, mwaka huu kwenye Robo Fainali ya kwanza ya michuano hiyo mipya inayosimamiwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika (ČAF).

Baada ya mchezo huo utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar, timu hizo zitarudiana Oktoba 24, mwaka huu nchini Misiri ambapo mshindi wa jumla anakwenda Nusu Fainali kukutana na mshindi kati ya Atlético Petróleos de Luanda na Mamelod Sundowns.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amesema watahangaika iwezekanavyo na Al Ahly Kwa Mkapa ili wamalize mchezo huo mapema.

“Al Ahly wanatufahamu vizuri vurugu zetu, hivyo Oktoba 20 mbele ya viongozi wa CAF na FIFA tutahakikisha tunaenda kuwashangaza na kuwapa furaha viongozi hao ili kutoboa kucheza hatua ya Nusu Fainali.

“Haya mashindano ni ya wakubwa na kwamba mtoto mwenye chini ya miaka 18 haruhusiwi kusogea, hivyo tumefurahi kupangwa na wakubwa wenzetu na hilo tulilijua mapema,” amesema Ahmed Ally

Makatibu SADC wakutana kwa dharula hali ya Ulinzi, Usalama
Mafuta yapaa, Wafanyabiashara wapewa angalizo