Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Forums, Maxence Melo kifungo cha nje cha mwaka mmoja na kumtaka kutokufanya kosa lolote la kijinai baada ya kupatikana na hatia ya kuzuia askari kutekeleza majukumu yao.

Katika shitaka la kwanza la kutosajili JamiiForums kwa kikoa cha DO-TZ, Maxence amekutwa hana hatia.

Katika shtaka la pili, Mahakama imemkuta na hatia na kumuachia kwa masharti ya kutofanya kosa kama hilo kwa muda wa mwaka mmoja.

Shtaka la pili lilihusisha Jeshi la Polisi kumtaka Maxence Melo kutoa taarifa za wanachama wa JamiiForums waliofichua uhalifu uliofanywa na baadhi ya wafanyakazi wa CRDB.

Pia, mahakama hiyo imemuachia huru Micke Mushi baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake.

Hukumu hiyo imetolewa leo Jumanne Novemba 17, 2020 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Huruma Shaidi, wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kusomwa hukumu.

Watanzania watatu washikiliwa Kenya
CECAFA U20 kuanza Arusha Nov 22

Comments

comments