Benki kuu ta Tanzania   (BOT), imechukua usimamizi wa China Commercial Bank Limited na kuisimamisha bodi ya wakurugenzi na uongozi wa benki hiyo kuanzia Novemba 19,2020.

Gavana wa BOT Prof. Frolens Luoga amesema kuwa uamuzi huo umefikiwa baada ya kubaini benki hiyo ina upungufu mkubwa wa mtaji, kinyume na matakwa ya sheria ya mabenki na taasisi ya fedha ya mwaka 2006 na kanuni zake

Prof. Luoga amesema kuwa upungufu huo unahatarisha usalama wa sekta ya fedha nchini, pamoja na usalama wa amana za wateja wa benki hiyo.

Aidha BOT imemteua maneja msimamizi ambae atakuwa na jukumu la kusimamia shughuli za benki hiyo kwa kipindi ambacho itakuwa chini ya BOT.

“Umma unaarifiwa kwamba katika kipindi kisichozidi siku 90, kuanzia siku ya taarifa hii, ( Novemba 19), shughuli za utoaji wa huduma za kibenki za China Commercial Bank Limited, zitasimama ili kuipa nafasi BOT kutathmini hatua za kuchukua, ili kupata ufumbuzi wa suala hili”. amesema Gavana BOT.

Prof. Luoga amehitimisha kwa kusema BOT itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana, katika mabenki kwa lengo la kuleta ustahimilivu katika sekta ya fedha.

Ukweli kuhusu Tanzania kufutiwa misaada na Bunge la Ulaya
Mtoto wa miaka 9 anusurika kuchinjwa na baba yake