Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa gawio la Shilingi Bilioni 300 kwa Serikali kutokana na faida iliyopatikana kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017.

Taarifa iliyotolewa na Benki Kuu imesema kuwa gawio hilo kutoka benki kuu kwenda Serkalini linafikisha jumla ya shilingi bil, 780  kwa kipindi cha miaka mitatu (2014/2015- 2016-2017),

Aidha, Katika taarifa hiyo iliyotolewa na Benki Kuu imesema kuwa majukumu ya msingi ya Benki hiyo siyo kutengeneza faida na inapotokea faida imepatikana, sehemu kubwa hutolewa kama gawio kwa serikali.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Sheria ya Benki Kuu ya mwaka 2006. jukumu kuu la benki kuu ni kuandaa na kutekeleza sera ya fedha inayolenga kudhibiti mfumuko wa bei na kujenga mfumo wa fedha ulio imara unaofaa kwa ukuaji endelevu na imara wa uchumi.

 

Waliopiga mali za CCM matumbo joto
Maneno: Wapinzani safari yao inaishia 2019- 2020