Boti kubwa ya MV Julius iliyokuwa inasafiri kutoka kisiwa kimoja kuelekea jijini Mwanza imezama Ziwa Victoria muda mfupi uliopita ikiwa na watu 17 na mzigo wa dagaa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi amesema kuwa watu wote waliokuwa kwenye boti hiyo wameokolewa na wako salama. Amesema kati ya watu hao, watano ni wafanyakazi wa boti hiyo.

Amesema kuwa chanzo cha boti hiyo iliyokuwa na gunia 250 za dagaa kuzama ni hitilafu iliyotokea muda mfupi baada ya kuanza safari na kusabanisha iegemee upande mmoja.

“Habari za awali zinaeleza kwamba wote wameokolewa, wako salama. Haikuwa mbali sana na pale kisiwani. Kwahiyo, ile hali ya mtumbwi kuwa inapata shida iilkuwa inaonekana mapema,” Kamanda Ollomi ameiambia ITV.

Ameseam kuwa ameagiza askari wa kikosi cha maji kufika katika tukio hilo mara moja na kutoa msaada zaidi.

Azam FC kuikabili Njombe Mji bila Himid Mao
Mbowe: Masha hakuwa na msaada wowote Chadema