Beki wa Kulia wa Young Africans Paul Godfrey ‘Boxer’ huenda akatolewa kwa mkopo katika kipindi hiki cha Dirisha Dogo la Usajili, huku klabu za Mtibwa Sugar na Polisi Tanzania zikitajwa kumuwania.

‘Boxer’ anatajwa kuwa kwenye mpango wa kuondoka kwa mkopo, kufuatia kukosa nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha Young Africans, baada ya usajili wa Kibwana Shomari aliyetua Jangwani tangu msimu uliopita 2020/21 akitokea Mtibwa Sugar.

Mpango wa kuondoka kwa mkopo klabuni hapo, umechagizwa na Kocha Mkuu Nesreddine Nabi, ambaye anaamini ‘Boxer’ ana nafasi ya kucheza kwenye kikosi chake kwa siku za usoni.

Katika hatua nyingine Kocha Nabi ameushauri Uongozi wa Young Africans kusitisha mpango wa kuachana na beki wa kushoto Adeyum Saleh katika kipindi hiki cha Dirisha Dogo la Usajili ili amuangalie na atatoa uamuzi kama aondoke au abaki baada ya kurejea kutoka mkoani Rukwa.

Mkataba wa Adeyum Saleh na Young Africans unakaribia kufikia ukingoni, hivyo juhudi zake zitaamua kama ataendelea kusalia klabuni hapo ama kuondoka.

Ruben Neves ampagawisha Thomas Tuchel
Sure Boy aigomea Azam FC