Beki wa kulia ya Yanga, Paul Godfrey ‘Boxer’ sasa yupo tayari kuiwakilisha timu hiyo katika mechi ya kimataifa dhidi ya Pyramids ya Misri.

Godfrey ambaye alikuwa majeruhi, amesema hivi sasa hali yake inaendelea vizuri na kuna uwezekano akawa sehemu ya mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramids Fc ya nchini Misri.

“Nipo fiti kwani mazoezi nilishaanza muda, nipo tayari kwa kuitumikia timu yangu kwa nguvu zangu zote kama ilivyokuwa zamani.

“Hata ikitokea kocha akanipatia nafasi ya kucheza dhidi Waarabu nipo tayari,” alisema Boxer ambaye kwa sasa ni mmoja kati ya mabeki wa kulia wanaofanya vizuri hapa nchini.

Yanga  ni timu  pekee iliyobakia katika michuano ya kimataifa kwa upande wa Tanzania ambapo imepangwa kucheza na Pyramids kwenye hatua ya Mtoano ya Kombe la Shirikisho ambapo mchezo wa awali unatarajiwa kupigwa oktoba 27 mwaka huu katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Rashford aibeba Manchester United kwa majogoo
Man City haipo tayari kutwaa ubingwa wa Ulaya – Guardiola