Mshambuliaji wa pembeni wa klabu bingwa nchini Ujerumani, FC Bayern Munich, Douglas Costa ameondolewa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Brazil ambacho kitapambana kwenye michuano ya Olimpiki itakayoanza mapema mwezi ujao mjini Rio de Janeiro.

Costa amelazimika kuwekwa pembeni kutokana na majeraha ya misuli ya paja yanayomsumbua.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25, alikua mmoja wa wachezaji watatu wenye umri zaidi ya miaka 23 waliotajwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Brazil ambacho kitakua na jukumu la kuhakikisha medali za dhababu haziondoki nyumbani.

Wengine walioteuliwa kwa kigezo cha kuzidi umri wa miaka 23 ni mshambuliaji wa FC Barcelona, Neymar pamoja na mlinda mlango wa klabu ya Palmeiras, Fernando Prass.

Brazil wataanza kampeni ya kuwania medali za dhahabu za Olimpiki, kwa kupambana na Afrika kusini katika uwanja wa Nacional Mane Garrincha uliopo mjini Brasilia, Ogasti 4.

Brazil imepangwa katika kundi A, sambamba na Afrika kusini, Iraq pamoja na Denmark.

Kundi B, lina timu za Sweden, Colombia, Nigeria pamoja na Japan

Kundi C, lina timu za Fiji, Korea Kusini, Mexico na Ujerumani

Kundi D, Honduras, Algeria, Ureno na Argentina.

Roma kuachia Video na Audio ya ‘Kaa Tayari’ Kesho, angalia kionjo hapa
Lil Wayne aandamwa na Kifafa, alazwa ICU