Brazil imeripoti visa vipya 33,274 vya Covid-19 ndani ya saa 24 na kufanya kuwa na jumla ya visa 499,966 ikiwa ni nchi ya pili kwa visa vingi zaidi nyuma ya Marekani ambayo ina visa zaidi ya milioni 1.8.
Nchi hiyo ya Marekani ya Kusini imerekodi vifo vipya 956 na kuwa na jumla ya vifo 28,849.
Orodha hiyo inafuatiwa na Ufaransa ambayo imerekodi vifo 28,771, ikiwa nyuma ya Marekani iliyorekodi vifo 105,230, Uingereza 38,376 na Italia vifo 33,340.
Magavana wa Majimbo wanajiandaa kulegeza masharti ya kuwazuia watu majumbani, lakini wataalam wa afya wameonya kuwa hali mbaya zaidi ya ugonjwa huo inakuja.
Rais wa Brazil, Jair Bolsonaro amekataa mpango wa kuwazuia watu majumbani (lock-down), akieleza kuwa hatua hiyo itaathiri kwa kiwango kikubwa uchumi.
WHO: Uongozi imara chanzo cha Afrika kupata maambukizi madogo ya corona