Watu sita wamefariki papo hapo katika ajali iliyohusisha Basi la Machame lililokuwa likitokea mkoani Dodoma kuelekea Arusha katika eneo la Kiongozi Wilayani Babati, Mkoani Manyara.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara Paul Kasabago amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo amesema waliofariki ni wanaume wanne na wanawake wawili ambao miili yao imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Babati ya Mrara mkoani humo.

Katika ajali hiyo watu kadhaa wamejeruhiwa ambapo chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana.

Mkuu wa mkoa wa Manyara Joseph Mkirikiti amefika katika eneo la ajali na kuwataka madereva kuwa waangalifu hasa katika kipindi hiki cha mvua.

Rais Samia afanya uteuzi
Ombi la BAVICHA kwa Rais Samia