Basi la Kampuni ya Saratoga lililokuwa likitoka Kigoma kuelekea Sumbawanga limewaka moto na kuteketea katika Kijiji cha Kazuramimba mkoani Kigoma.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma, Martin Otieno amesema kuwa basi hilo limeteketea kwa moto na lilikuwa na abiria 60 ambao wamefanikiwa kutoka wote wakiwa salama, pia baadhi ya mizigo imeokolewa.
Kamanda amesema kuwa basi hilo lililokuwa linatokea Kigoma Mjini kuelekea Sumbawanga limeteketea lote kwa moto na hadi sasa wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha moto huo
Endelea kuwa nasi kwa taarifa zaidi.