Miili ya watoto wawili imeopolewa katika shimo lililodaiwa kuwa ni shimo la choo eneo la Mji Mpya katika Mtaa wa Olkerian jijini Arusha. Shimo hilo lipo kwenye nyumba ambayo ujenzi wake haujakamilika.

Tukio hilo limethibitishwa na mwenyekiti wa mtaa huo uliopo Kata ya Olasiti, Daudi Safari ambapo ameeleza kutokea kwa tukio hilo la kukutwa miili ya watoto wawili ambayo haijatambuliwa bado. Wakazi wa jiji la Arusha waliokusanyika kwenye nyumba ambayo ujenzi wake haujakamilika kushuhudia uopoaji wa miili ya watoto hao.

Kazi hiyo ya uopoaji imetekelezwa na  Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Jeshi la Polisi na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

 

Magazeti ya Tanzania leo Septemba 6, 2017
Wananchi wateketeza mali za familia 6 kwa tuhuma za ushirikina