Aliyekuwa Mwenyikiti wa ACT-Wazalendo  ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mgwhira mapema leo hii ametangaza kujiunga na CCM alipokuwa katika Mkutano wa 9 wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT.

Mghwira amesema kuwa ameridhika na mwenendo mpya wa Chama hicho chini ya Mwenyekiti wake, Dkt John Pombe Magufuli.

”Nimeiona CCM inayobadilika, nimeona juhudi za kila mtu, ninaiona CCM inayoanza kukataa rushwa, nimeiona CCM inayoanza kulipeleka taifa mbele” amesema Anna Mghwira.

Mnamo Juni 3, 2017 Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania alimteua Anna Elisha Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Mghwira alikuwa mgombea pekee wa kike wakati wa kinyang’anyiro cha urais mwaka 2015, kwa tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo na amekuwa mwenyekiti wa chama hicho tangu kilipoundwa mwaka 2014.

 

 

Ronaldo atwaa tuzo mchezaji bora wa dunia 2017
Maharamia kazi za filamu kufikishwa mahakamani