Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema Kamati Kuu ya Chama hicho iliyoketi Nov 27,2020 imeazimia kuwavua uanachama Halima Mdee na wenzake 18 walioapishwa Novemba 24, kuwa Wabunge Viti Maalum.

“Chama chetu hakijateua Wabunge wa Viti Maalum tunaona tu Watu wetu wanaapishwa na hatuna taarifa, hatujapeleka majina, fomu za Tume zipo ofisini, Mama zetu hawa Dada zetu hawajajaza fomu, ila tunaona tu wanaapishwa, wamekinajisi Chama na wamekataa kuja kwenye Kamati Kuu” amesema Mbowe.

“Kamati Kuu imewavua Uongozi wale wote ambao walikuwa viongozi kwenye mabaraza kati ya hao Dada zetu 19, sitaki kupoteza muda kuwataja majina, kwahiyo kuanzia sasa hawapaswi kushughulika na lolote kama viongozi na tumeelekeza nafasi zao zizibwe haraka” ameongeza Mbowe.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Novemba 29, 2020
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Novemba 28, 2020