Shirikisho la soka duniani FIFA, limetangaza kumtimua kazi katibu mkuu Jerome Valcke, ambaye alikua akikabiliwa na tuhuma za udanganyifu na ufisadi.

Kamati ya utendaji ya shirikisho hilo, imefikia maamuzi hayo, baada ya kujiridhisha na tuhuma zilizokua zikimkabili kiongozi huyo ambaye ilionekana alihusika na sehemu ya ufisadi ambao ulikua ukiendelea.

Valcke, alisimamishwa kazi tangu Oktoba 8 mwaka jana ili kupisha uchunguzi uliokua ukiendelea dhidi yake.

Hata hivyo kikao cha kamati ya utendaji ya FIFA kilichoketi Januari 09 mwaka huu, kilianza kujadili suala la katibu huyo kutoka nchini Ufaransa kabla ya muda mchache uliopita kutoa taarifa za kumtimua.

Taarifa iliyotolewa  kwenye tovuti ya FIFA inasomeka “FIFA imefikia maamuzi ya kumtimua kazi Jerome Valcke katika nafasi yake ya ukatibu mkuu, na nafasi hiyo kwa sasa haitojazwa mpaka hapo taratibu zitakapotangazwa.”

Valcke amekua katika utumishi wa FIFA kama katibu mkuu, tangu mwaka 2007 na mara kadhaa amekua akikanusha kuhusika na masuala mbali mbali ya udanganyifu ambao alidaiwa kuufanya na kupelekea ufisadi mkubwa kujitokeza.

Louis Van Gaal Awalaumu Wachezaji Wa Man Utd
Mkwasa Awapa Dozi Ya Siku 1 Makocha Zanzibar