Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema) kimepata pigo tena baada ya Mbunge wao wa Serengeti mkoa wa Mara, Marwa Ryoba kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge na kujiunga na chama cha Mapinduzi (CCM).

Marwa amejiuzulu leo Septemba 28, 2018 ambapo moja ya sababu za uamuzi huo ni kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Pia, Diwani wa Chadema kata ya Nkoanekoli halmashauri ya wilaya ya Meru, Wilson Nanyaro naye ametangaza kujiuzulu kama ilivyo kwa Marwa na kujivua uanachama wa Chadema na kujiunga na CCM kwa sababu zile zile za kumuunga mkono Rais  Dkt. John Pombe Magufuli.

Chadema wamjibu Makonda kuhusu 'Flyover'
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Septemba 28, 2018