Mbunge wa Jimbo la Simanjiro kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), James Ole Millya ametangaza rasmi leo kujiuzulu nafasi zake zote za uongozi ndani ya chama hicho na kuomba kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Millya ambaye alijiunga na Chadema miaka sita iliyopita akitokea CCM amekuwa mbunge wa nne kutoka chama hicho kuondoka na kujiunga na CCM huku naye akisema ameamua kujizulu kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kuwatumikia wananchi.


Video: MKASA HUU UTAKUTOA MACHOZI: Amempa sumu mtoto wake na yeye mwenyewe amejiua | Mtoto amenusurika

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Oktoba 8, 2018
Video: Changamoto ya ajira yazidi kupungua nchini