Ndege ya shirika la ndege la Emirates iliyokuwa ikitoka nchini India imeanguka wakati inatua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Dubai ikiwa na abiria 275, pamoja na wafanyakazi kadhaa wa ndege hiyo.

Shirika la habari la Serikali la Dubai (Falme za Kiarabu), limetoa taarifa kupitia mtandao wa twitter kuwa abiria wote wameokolewa kutoka kwenye ndege hiyo na hakuna hata mmoja aliyejeruhiwa.

“Kipaumbele chetu hivi sasa ni usalama wa wahanga wote wa ajali hii,” uongozi wa Emirates uliandika kwenye mtandao wa Twitter.

Kufuatia tukio hilo, ratiba ya ndege zote zilizokuwa zinapaswa kuondoka au kutua katika uwanja huo wa ndege ilisitishwa kwa muda wakati kikosi maalum cha masuala ya dharura kikiendelea na huduma.

Chanzo cha ajali hiyo bado hakijabainishwa.

Mchungaji afariki akijaribu kushindana na Yesu kufunga
Madaktari wasahau taulo ndani ya tumbo la Mgonjwa baada ya upasuaji