Aliyekuwa Rais wa Sudan, Omar al – Bashir ametolewa madarakani baada ya kutawala nchi hiyo kwa miaka 30.
Polisi mjini hapo wamezunguka makazi ya rais huyo vyanzo vya habari vinasema Majeshi ya Sudan yamedhibiti nchi huku Rais Omar al-Bashir akilazimishwa kujiuzulu kwa lazima na kutoka nje ya Ofisi ya Ikulu.
“Jeshi nchini hapa (Sudan), limetangaza kumuondoa madarakani Rais Omar al-Bashir. Mamia ya wanajeshi wametanda katika makazi rasmi ya rais tokea alfajiri ya leo,” kuna taarifa zinazoeleza pia kuwa baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali, wamekamatwa na jeshi na uwanja wa ndege jijini Khartoum umefungwa, Anasema mwandishi habari mashuhuri nchini Sudan” Yousra Elbagir.
Hali hii inakuja katikati ya maandamano dhidi ya Rais Omar al-Bashir ambayo yamechukua miezi kadhaa sasa.
Tayari uwanja wa ndege wa Khartoum, Sudan umedhibitiwa na Jeshi.
Baadhi ya viongozi wa juu wa Serikali akiwemo Waziri wa zamani wa Ulinzi na Kiongozi wa juu wa Chama tawala wanashikiliwa na Jeshi..
Kabla ya hatua hiyo ya jeshi, wananchi walipanga kuendelea na maandamano yao ya kushinikiza rais huyo kuondoka madarakani.
Maandamano dhidi ya al-Bashir yalianza Desemba mwaka jana, ambako wananchi waliingia barabarani kupinga kupanda kwa bei ya vyakula.
Hata hivyo, kadri muda ulivyosogea, ndivyo maandamano hayo yalivyozidi kuwa makubwa na kubadili lengo lake halisi la kupinga ongezeko la chakula na kuelekezwa kwenye “kumng’oa rais Bashir madarakani.”
Taarifa zinasema, magari yaliyosheheni wanajeshi wenye silaha yameegeshwa kwenye barabara zote muhimu na madaraja kwenye mji mkuu, shirika la habari la Reuters linanukuu mashuhuda.