Saa chache baada ya kutangazwa kwa bei mpya za vifurushi, Serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), imesitisha gharama mpya za vifurushi hadi hapo baadae na kuagiza vifurushi vya zamani kuendela kutumika.

Uamuzi huo unaweza kuwa habari njema kwa watumiaji wa mitandao ya simu ambao, tangu kutangazwa kwa bei hizo mpya mapema leo Ijumaa ya Aprili 2, 2021, wamekuwa kwenye mjadala mzito kwani, matarajio ya wengi ilikuwa ni kushuka kwa gharama hizo.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Semu Mwakyanjala, amesema matumizi ya bei mpya ya vifurushi yamesitishwa kwa muda.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Aprili 3, 2021
G7 yawashukia wanajeshi wa Eritrea