Kocha wa klabu ya Celtic, Brendan Rodgers ameweka rekodi ya kuwa kocha wa kwanza kuifanya timu kutoka Uingereza kucheza michezo 63 ya ligi ya ndani bila kupoteza.

Celtic wameshinda michezo 56 na kusuluhu michezo 7 wakiwa wamefunga mabao 183, wakifungwa mabao 35 na kucheza michezo 36 bila nyavu zao kuguswa.

Hata hivyo pamoja na Rodgers kuwapa Celtic rekodi hiyo tayari kuna vilabu ambavyo vimecheza mechi nyingi zaidi katika ligi zao bila kupoteza mchezo hata mmoja.

Vilabu vingine ambavyo vimecheza mechi nyingi zaidi katika ligi zao bila kupoteza mchezo hata mmoja ni pamoja na;

1.Steaua Bucharest. Hakuna klabu dunianj inayofikia rekodi ya timu hii kutoka Romania,mwaka 1986 wakati wakibeba kikombe cha European Cup walicheza michezo 119 ya ndani hadi mwaka 1989 ndipo wakapoteza mchezo.

2.Lincolin Red Imps. Mwaka 2009 mwezi May hadi September mwaka 2014 walicheza michezo 88 ya ligi ya kwao bila kupoteza mechi na pia wamewahi kuchukua makombe 14 mfululizo ya ligi nchini kwao Gibraltar.

3.Ac Millan. Kati ya mwaka 1991 na 1993 klabu soka ya Ac Millan ilichukua makombe matatu mfululizo, lakini si hivyo tu bali pia Millan walicheza michezo 58 ya ligi ya kwao bila kupoteza hata mmoja.

4.Ajax. Ajax iliyochukua ubingwa wa Champions League mwaka 1995 ilikuwa kati ya Ajax bora kuwahi kutokea,mwaka ambao wanachukua kombe hilo walicheza michezo 52 bila kupoteza mchezo hata mmoja.

5.Arsenal. Wengi wanaikumbuka Arsenal hii ya nwaka 2003 ambapo hadi inafima 2004 mwezi October walikuwa hawajapoteza mchezo na Manchester United ndio walikatisha safari yao ya michezo 49 bila ushindi

Magazeti ya Tanzania leo Novemba 6, 2017
Liverpool wamelamba dume kwa Salah